Romans 12:4-8

4 aKama vile katika mwili mmoja tulivyo na viungo vingi, navyo viungo vyote havina kazi moja, 5 bvivyo hivyo na sisi tulio wengi, tu mwili mmoja katika Al-Masihi, nasi kila mmoja ni kiungo cha mwenzake. 6 cTuna karama zilizotofautiana kila mmoja kutokana na neema tuliyopewa. Kama ni unabii na tutoe unabii kwa kadiri ya imani. 7 dKama ni kuhudumu na tuhudumu, mwenye kufundisha na afundishe, 8 ekama ni kutia moyo na atie moyo, kama ni kuchangia kwa ajili ya mahitaji ya wengine na atoe kwa ukarimu, kama ni uongozi na aongoze kwa bidii, kama ni kuhurumia wengine na afanye hivyo kwa furaha.

Alama Za Mkristo Wa Kweli

Copyright information for SwhKC